Prof Elliot C Phiri, Rasi wa Ndaki ya CVMBS
Katika mashindano hayo yaliyotamatishwa leo, timu na mtu mmoja mmoja kutoka Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya wametia fora kwa kushinda katika michezo mbalimbali
Profesa Elliot E. Phiri ambaye ni Rasi wa Ndaki ameongoza wanandaki wake kwa kuibuka kidedea katika mbio na kukimbiza kuku. Katika mbio za mita 100 Prof Phiri ametimua mbio na kumaliza kwa sekunde 13 akiwaacha wenzake na kujishindia medali ya dhahabu.
Aidha, katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya SUA iliyoongozwa na Prof Phiri na Prof Karugila imezibwaga timu za NMB na CRDB na kuibuka kidedea.
Kwenye kandanda, timu ya CVMBS ilimenyana vilivyo na kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya NBM, na baadae wakajikuta wakichabangwa goli 2-1 na CRDB.
Funga kazi sasa ni pale Prof Phiri alipohakikisha kwenye kufukuza kuku anatimua mbio na kutumia mbinu za uwindaji alizojifunza huko Mbeya na kujikamatia jogoo wake mkubwa kabisa, ama hakika leo ataenda kupooza uchovu wa michezo kwa kitoweo safi sana.
Tunazipongeza timu zote za Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya na kwa namna ya pekee tukimpongeza Rasi wetu, Prof Phiri.