Kampeni ya kutokomeza kichaa cha mbwa kwa uchanjaji iliyoanza tarehe 6 May 2021 wilayani kisarawe inaendelea kwa ufanisi mkubwa.
Timu za wataalamu zimetawanyika sehemu mbali mbali za wilaya hiyo ambapo mwamko wa wananchi ni mkubwa kushiriki zoezi hilo.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Ms Jokate Mwegelo amekuwa bega kwa kweba na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kuhakikisha huduma zoezi hilo linaenda vyema.
Kabla ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo mnamo tarehe 6 May 2021, kulifanyika seminar maalumu kwa ajili ya kuwanoa wanafunzi wa Udaktari wa Mifugo na Udaktari wa Binadamu kutoka katika vyuo vya SUA na MUHAS mtawalia. Wanafunzi hao wapatao takribani 50 wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo chini ya uangalizi wa wataalamu kutoka katika vyuo hivyo viwili.
Tutakuwa tunawaletea hapa chini matukio mbalimbali yanayoendelea katika kampeni hiyo kwa njia ya picha
SIKU YA 4 – UCHANJAJI UNAENDELEA
Kuelimisha jamii
SIKU YA 3 – UCHANJAJI UNAENDELEA
Ms Jokate Mwegelo (Mkuu wa Wilaya Kisarawe) akishiriki zoezi la uchanjaji
SIKU YA 2 – UZINDUZI
SIKU YA 1 – MAFUNZO