TOKOMEZA KICHAA CHA MBWA: CVMBS WASHIRIKIANA NA WADAU KATIKA KAMPENI KUBWA YA KITAIFA

Kisarawe 1

Kisarawe 1

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Ms Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa SUA wanaoshiriki kampeni ya chanjo ya kichaa cha mbwa

Wataalamu na wanafunzi wa Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya wameungana na wadau wengine katika kampeni ya kitaifa ya kutokomeza kichaa cha mbwa kwa kuchanja mbwa na paka.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Ms Jokate Mwegelo tarehe 6 May 2021, inalenga kutoa chanjo kwa mbwa na paka wote nchini. Zaidi ya mbwa 2000 wanatarajiwa kuchanjwa wilayani humo.

SUA inashirikiana na wadau wengine katika kampeni hiyo wakiwemo MUHAS, AFROHUN na Mkurugenzi wa Tiba ya Mifugo nchini. Kampeni ya kutokomeza kichaa cha mbwa itasambazwa nchi nzima.

Miongoni mwa wataalamu wa SUA wanaoshiriki kwenye kamoeni hiyo ni Dr Athanas Ngou, Dr Richard Samsoni, Dr Khadija Said Majid Majid, Dr Albert Felix na wanafunzi 30 wa mwaka wa tano, Tiba ya Mifugo.

Kisarawe 2

Kichaa cha Mbwa ni ugonjwa unaosababishwa na virus wajulikanao kama Lyssavirus kutoka katika jamii ya virusi ya Rhabdoviridae. Ugonjwa huu ni miongoni  mwa mgonjwa yanayoambulizwa kati ya binadamu na wanyama (zoonotic diseases). Binadamu huambukizwa ugonjwa huu kwa kuumwa na mbwa au mnyama mwingine mwenye ugonjwa.

Virusi wa kichaa cha mbwa wanapoingia mwilini husafiri kupitia neva za fahamu hadi kwenye ubongo na kusababisha maradhi makali nap engine kifo.

Watu wanashauriwa kujingika na maambukizi kwa kuwaepuka mbwa wanaozurura hovyo hasa wanaoonekana kuwa na dalili za maambukizi. Inashauriwa wafugaji wahakikishe mbwa nap aka wao hawazururi ovyo mtaani na pia kuhakikisha wanapatiwa chanjo ya kichaa cha mbwa kila mwaka.

Endapo mbwa mwenye dalili za kichaa (kutokwa mate mengi mdomoni, kushambulia na kuuma watu, wanyama au vitu ovyo, na kuwa mkali) inashauriwa watu wasimsogelee na watoe taarifa kwa wataalamu wa mifugo mara moja.

Related Posts