Sio jambo la ajabu kukuta watoto ndio wanakuwa karibu sana na wanyama wa kufugwa hasa tunaowaita companion animals mfano mbwa na paka
Kuna wakati watoto wanakuwa karibu sana na wanyama hawa kiasi cha kuumia sana pale mnyama anapopata matatizo. Zipo familia ambazo mtoto anaweza kuwa rafiki na mbwa kiasi kwamba anaweza kumgawia chakula chake.
Ukaribu wa watoto na wanyama unatakiwa utukumbushe mambo mawili; kwanza umuhimu wa kuwapa watoto nafasi ya kuwatunza na pili kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka ka wanyama.
Kwa mantiki hiyo, wazazi wanapokuwa na wanyama companion nyumbani ni muhimu kuhakikisha wanapatiwa chanjo zote muhimu ikiwemo ya kichaa cha mbwa na dawa za minyoo kadiri wanavyoshauriwa na wataalamu. Hii itasaidia sana kuwalinda watoto na pia kuwapa wanyama matunzo mazuri.